Waziri wa Afrika Kusini atarajia kusafirisha brandy katika soko la China
2021-12-07 09:46:58| cri

Waziri wa Kilimo wa Afrika Kusini Ivan Meyer katika jimbo la Cape Magharibi, ambalo ni eneo kuu la uzalishaji pombe ya brandy ya Afrika Kusini amesema jimbo lake linatarajia kupata masoko mapya nchini China kwa ajili ya brandy yake “bora duniani”.

Bw. Meyer amesema wako tayari kuingia kwenye soko la China kwani nchi hii ina watu wengi, na Wachina wanapenda pombe kali ikiwemo brandy. Amefafanua kuwa Cape Magharibi imeanzisha uhusiano na wenzao wa China katika ngazi ya jimbo pamoja na uhusiano wa usafirishaji nje na China ambao una historia ndefu.

Amebainisha kuwa jimbo lake ambalo linauza nje bidhaa za kilimo kwa asilimia 53 ya nchi hiyo, tayari limeshasafirisha zabibu, matunda jamii ya machungwa na bidhaa nyingine za kilimo nchini China, na China ina jukumu muhimu kwenye nyanja ya kilimo katika kufufua uchumi wa Cape Magharibi kufutia athari za COVID-19.