Rais Xi Jinping wa China asisitiza kushikilia sheria za ujamaa wenye umaalumu wa China
2021-12-08 08:56:26| cri

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Xi Jinping amesisitiza kushikilia njia ya sheria za ujamaa wenye umaalumu wa China.

Xi amesema hayo katika Mkutano wa Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya CPC.

Pia amebainisha kuwa China sasa iko katika hatua muhimu ya kutimiza ufufuaji wa taifa, na kuhimiza juhudi za kuinua uwezo na kiwango cha utawala wa kisheria kwa pande zote, pamoja na kutoa uhakikisho thabiti wa kisheria kwa ajili ya kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa kwa pande zote.

Akitambua mafanikio ya kihistoria katika ujenzi wa mfumo wa utawala wa kisheria wa ujamaa wenye umaalumu wa China tangu Kamati Kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), rais Xi amesisitiza kuwa China imeanza safari mpya, ambayo imeleta mahitaji mapya na ya juu zaidi kwa utawala wa kisheria.

Pia ameongeza kuwa mfumo wa utawala wa kisheria wa ujamaa wenye umaalumu wa China unapaswa kuendelezwa kwa kina ili kuelekea upande sahihi katika kujenga mfumo wa kisheria, kudumisha uongozi wa Chama na mfumo wa ujamaa wenye umaalumu wa China, na kutekeleza nadharia ya utawala wa kisheria ya ujamaa ya China.