Rais wa China atoa pongezi kwa maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika
2021-12-09 14:51:55| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kwa njia ya simu kwa rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania akipongeza maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika.

Rais Xi amesisitiza kuwa kutokana na juhudi za serikali za Tanzania na wananchi wake wote, ujenzi wa taifa wa Tanzania umepata maendeleo makubwa na mafanikio mengi. Amesema China na Tanzania zimejenga na kuendeleza urafiki wa kina, na katika miaka ya hivi karibuni, uaminifu wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili umezidi kuimarika, na ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali umezidishwa. Rais Xi amesema anatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na anapenda kushirikiana na rais Samia kuhimiza uhusiano wa wenzi na ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote katika kiwango cha juu zaidi.