China na Rwanda zasaini makubaliano ya kuondoa ulipaji kodi mara dufu
2021-12-09 12:30:30| cri

China na Rwanda zimesaini makubaliano ya kuondoa ulipaji kodi mara dufu kwa kodi za Mapato na Kuzuia Ukwepaji Kodi pamoja na taratibu zinazohusiana nazo.

Makubaliano hayo yalisainiwa Kigali juzi Jumanne na balozi wa China nchini Rwanda Rao Hongwei na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Uzziel Ndagijimana. Baada ya kusaini balozi Rao alisema ushirikiano kwenye masuala ya kodi kati ya nchi mbili una umuhimu mkubwa katika kufanya uhusiano wa kibiashara wa pande mbili uendelee vizuri na kudumu. Kusainiwa kwa makubaliano hayo pamoja na taratibu zake nyingine kutapunguza sana mzigo wa kodi wa walipa kodi wanaowekeza katika pande zote mbili na kusukuma mbele ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa pande mbili pamoja na mabadilishano ya wafanyakazi.

Naye Ndagijimana amesema makubaliano hayo yataboresha nafasi ya Rwanda kama sehemu nzuri ya uwekezaji kwa makampuni ya China.