Africa CDC:Nchi 11 za Afrika zaripoti virusi vilivyobadilika vya COVID-19 aina ya Omicron
2021-12-10 09:14:24| cri

Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) Bw. John Nkengasong ametangaza kuwa hadi sasa nchi 11 za Afrika zimeripoti wagonjwa wa COVID-19 wenye virusi vya Omicron, zikiwemo Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, Ghana, Uganda, Zambia, Senegal, Tunisia, Msumbiji, Namibia na Zimbabwe.

Umoja wa Afrika (AU) umeonya kwamba marufuku ya kusafiri na kuingia inayohusiana na kuibuka kwa virusi vya Omicron inazuia usafirishaji huru wa watu na bidhaa, na kuleta athari za haraka na kubwa kwa nchi za Afrika.

Umoja wa Afrika wenye wanachama 55 ulitoa wito wa kuondolewa haraka marufuku ya kusafiri iliyowekwa katika nchi za kusini mwa Afrika kufuatia kugunduliwa kwa Omicron.

Ushahidi uliopo, ambao unasisitiza kuenea na kusambaa kwa virusi vya Omicron duniani na kwenye jamii, hauna mashiko kwenye upande wa marufuku hiyo ya kusafiri iliyowekewa nchi za Kusini mwa Afrika.