UM: Mashirika ya misaada yanaendelea kupeleka misaada kaskazini mwa Tigray licha ya kukabiliwa na changamoto
2021-12-10 09:13:56| cri

Umoja wa Mataifa na washirika wake wanaendelea kusambaza misaada ya kibinadamu kaskazini mwa Ethiopia wakati ambapo makumi kwa maelfu ya watu wamepoteza makazi na misaada kuzuiwa.

Kwenye ripoti yake Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema kuna ongezeko kubwa la vurugu zinazosababisha watu kukimbia makazi katika mkoa wa Tigray, ambazo zimesambaa hadi mkoa wa Amhara uliopo kusini na Afar wa mashariki, na baadhi ya wakati zinafika hadi kati ya Amhara na Afar.

OCHA imesema katika siku saba za mwanzo za mwezi Disemba malori 44 ya chakula, vitu vya lishe, maji na vifaa vya usafi yalifika Mekelle mji mkuu wa Tigray kupitia ushoroba wa Afar, ambapo idadi ya sasa ya malori ya misaada ni ndogo sana ikilinganishwa na idadi ya awali ya malori 157 kwa wiki, kwani yanahitajika malori 100 kwa siku ili kufikia mahitaji ya Tigray. Hata hivyo OCHA imesema licha ya idadi hiyo kupungua mashirika ya misaada yanaendelea kupeleka msaada wa kuokoa maisha na huduma za lazima huko Tigray.