Tanzania bara yaadhimisha miaka 60 ya uhuru
2021-12-10 09:13:29| cri

Tanzania bara Alhamis ya tarehe 9 Disemba iliadhimisha miaka 60 ya uhuru kwa vifijo na nderemo huku viongozi na wawakilishi mbalimbali kutoka nchi nyingi za nje wakijiunga kwenye maadhimisho hayo.

Viongozi waliohudhuria kwenye sherehe hiyo ya kufana iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ni kutoka Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, Comoro, Msumbiji, DRC, Eswatini, Oman, Malawi na nyingine nyingi za Afrika. Wakati anawasili kwenye Uwanja wa Uhuru rais wa Tanzania na Amiri jeshi mkuu Samia Suluhu Hassan alipokelewa na mizinga 21 na kupigiwa wimbo wa taifa wa Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, na baadaye alikagua gwaride la heshima.

Wakati akilihutubia taifa Jumatano kwa ajili ya maadhimisho hayo, rais Samia aliwataka Watanzania kuendelea kuilinda nchi kwa kuendeleza amani, mshikamano na maelewano. Amesema kwa miaka yote 60 ya uhuru nchi imefanikiwa kulinda uhuru na mipaka yake.