Kenya yaanzisha mpango wa miamala ya pesa taslimu ili kuwasaidia watu wanaokumbwa na ukame
2021-12-10 09:13:02| cri

Kenya jana ilianzisha mpango wa dharura wa miamala ya pesa taslimu kupitia jukwaa la kufanya miamala ya pesa kwenye simu za mkononi, ili kuwasaidia watu wanaokumbwa na ukame na kuboresha maisha yao.

Waziri wa Utumishi wa Umma, Jinsia, Wazee na Mipango Maalumu wa Kenya Margaret Kobia amesema katika awamu ya kwanza familia 360,696 zitapewa pesa hizo, na kila familia itapata shilingi 3,000 (sawa na dola takriban 26.57 za kimarekani) kila mwezi hadi hali ya mvua itakapokuwa nzuri.

Ameongeza kuwa kubadilisha kutoka usambazaji wa chakula na kufanya miamala ya pesa taslimu kutaongeza ufanisi wa kazi za kibinadamu, hatua ambayo imethibitishwa kuwa ni njia yenye ufanisi zaidi katika kuwasaidia watu chini ya hali ya dharura, na inaweza kuhakikisha heshima ya watu wanaopewa msaada na kuchochea uchumi wa huko.