Wagonjwa zaidi ya 37 wa kipindupindu waripotiwa katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania
2021-12-13 10:46:51| CRI

Wagonjwa zaidi ya 37 wa kipindupindu wameripotiwa katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Ofisa mkuu wa afya wa kanda ya Nkasi Bw. Benjamin Chota amesema, kikundi cha kwanza cha wagonjwa watatu wa kipindupindu waliripotiwa Desemba 2 katika zahanati ya kata ya Korongwe.

Bw. Chota amesema baada ya kuripoti wagonjwa hao watatu, timu ya wataalamu wa afya ilikusanya sampuli kutoka wagonjwa hao na upimaji umeonesha kuwa wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu.

Amesema serikali ya Nkasi imejenga kituo cha muda kuwatibu wagonjwa 37, ambacho hadi kufikia Desemba 10 wagonjwa 37 walikuwa wamepata matibabu.