Rais wa Afrika Kusini aambukizwa COVID-19
2021-12-13 08:59:27| CRI

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini anapata matibabu baada ya kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona yenye dalili ndogo.Kwa mujibu wa Ikulu ya Afrika Kusini, rais Ramaphosa aliyepewa dozi kamili za chanjo ya COVID-19, alianza kutojisikia vizuri mapema Jumapili. Kwa sasa rais huyo yuko katika hali nzuri chini ya ufuatiliaji wa Idara ya Huduma za Afya ya Jeshi la Afrika Kusini.

Rais Ramaphosa amethibitishwa kuambukiziwa muda mfupi baada ya kumaliza ziara katika nchi nne za Afrika Magharibi, zikiwemo Nigeria, Cote d’Ivoire, Ghana na Senegal.

Rais Ramaphosa alisema kuambukizwa kwake kunatoa tahadhari kwa watu wote nchini humo wapate chanjo na wawe makini na hatua za kujikinga.