Serikali ya Zimbabwe imesema inaunga mkono kikamilifu michezo ya olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing ya mwaka 2022, na kupinga majaribio yoyote ya nchi za magharibi kuingiza mambo ya kisiasa kwenye michezo hiyo.
Waziri wa habari, uenezi na utangazaji wa Zimbabwe Bibi Monica Mutsvangwa amesema michezo inatakiwa kuwa michezo na isifanywe kuwa siasa. Amesema Zimbabwe inaitakia China kila la heri, na Beijing kila mafanikio, wakati inaandaa michezo hii kukiwa na kivuli cha janga la COVID-19. Amesema China ina uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Amesema michezo hiyo itakuwa mizuri kwa wanamichezo wote waliojiandaa kwa ajili ya michezo hiyo, na watu duniani watatazama kwenye televisheni na kuburudika kwa michezo hiyo.