Rais Kenyatta atangaza kupunguza bei ya umeme Kenya kwa asilimia 30 ili kuhimiza maendeleo ya viwanda
2021-12-13 09:28:16| CRI

Kenya inapanga kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 30 ili kuondoa shinikizo la mfumuko wa bei kwa wananchi wake na kuhimiza ongezeko la uchumi kwa sekta ya viwanda nchini Kenya.

Akiongea kwenye siku ya Uhuru ya Kenya, Bw. Kenyatta amesema kupunguza bei ya umeme kutafanyika katika hatua mbili za asilimia 15, ikiwa ni hatua ya kutekeleza ahadi aliyoitoa mwezi Oktoba kuwalinda watumiaji na wanaviwanda dhidi ya gharama kubwa za umeme. Upunguzaji huo wa bei utakamilika katika robo ya kwanza ya mwaka kesho.

Kwenye hotuba yake kwa taifa Rais Kenyatta amewataka wazalisha umeme kuonyesha nia njema kufanya sekta ya nishati kuwa kichocheo cha maendeleo ya taifa.