DRC kuweka muda wa ukomo wa uwepo wa vikosi vya Uganda kwenye ardhi yake
2021-12-14 09:02:25| CRI

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) jana alisema ameweka muda wenye ukomo wa uwepo wa majeshi ya Uganda kwenye ardhi ya nchi yake.

Akihutubia taifa kupitia bunge mjini Kinshasa, kwa mara ya kwanza Rais Tshisekedi amekiri kuwepo kwa operesheni ya pamoja, na uwepo wa majeshi ya Uganda kwenye ardhi ya DRC, na kusema waasi wa ADF ni adui wa pamoja wa nchi hizo mbili. Amesema bunge linafahamu kuhusu uwepo wa jeshi hilo, na yeye ataweka ukomo wa operesheni za pamoja na uwepo wa jeshi la Uganda kwenye ardhi ya DRC.

Kwa mujibu wa mamlaka za nchi hizo mbili, kwa sasa wanajeshi 1,700 wa Uganda wako nchini DRC, wakiwa pamoja na magari 100 ya kusafirisha wanajeshi, pamoja na vifaru.