Mji wa Cape Town kupiga marufuku magari katika maeneo ya migahawa kuhakikisha usalama
2021-12-14 09:01:20| CRI

Mji wa Cape Town wa Afrika Kusini umetangaza kuwa utazuia magari kupita kwenye baadhi ya barabara mjini Cape Town ili kuweka mazingira mazuri ya nje kwa watu wanaopenda kula chakula nje.

Hatua hiyo ina lengo la kuisaidia migahawa katika majira ya joto, kipindi ambacho kina watalii wengi, ili kuunga mkono sekta ya utalii na huduma ambayo imeathiriwa kutokana na kukatishwa kwa ghafla kwa safari za kimataifa kufuatia kugunduliwa kwa virusi aina ya Omicron.

Meya wa mji wa Cape Town Bw Geordin Hill-Lewis amesema hatua inatarajiwa kuwasaidia watu wanaofanya kazi kwenye sekta ya huduma.

Hatua nyingine iliyochukuliwa na mji huo wiki iliyopita ni kupunguza gharama za tiketi za ndege, malazi na tiketi za maeneo ya vivutio ili kuvutia watalii wa ndani.