Polisi Kenya wazuia utekaji nyara wa raia 40 kwenye eneo la mpaka
2021-12-14 09:05:40| CRI

Polisi nchini Kenya jana Jumatatu walizuia jaribio la wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab kuwateka nyara waumini katika msikiti mmoja huko Konton katika kaunti ya Wajir kwenye mpaka wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Wajir Hilary Toroitich amesema kikundi cha watu watano kilivamia msikiti huo na kuwateka nyara waumini wapatao 40 waliokuwepo.

Bw. Toroitich amesema wanamgambo hao wanaoshukiwa kutoka Somalia waliwaamuru waumini kutoka msikitini na kuingia kwenye kichaka kuelekea kwenye mpaka kati ya Kenya na Somalia, kabla ya kukimbia kufuatia kufyatuliwa risasi na polisi. Amesema hakuna ripoti ya vifo au majeruhi kwenye tukio hilo.