Watu 9 wafariki katika ajali ya barabarani kusini mwa Tanzania
2021-12-14 09:20:28| cri

Watu wasiopungua tisa wamefariki papo hapo na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya gari moja la kubeba magazeti kugonga mti Jumatatu wiki hii huko Iringa, kusini mwa Tanzania.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bw. Allan Bukumbi amesema ajali hiyo ilitokea kwenye barabara ya Dar es Salaam-Mbeya katika kijiji cha Mahenge cha wilaya ya Kilolo, baada ya dereva wa gari hilo kushindwa kulidhibiti kwenye kona kali.

Alisema marehemu waliokufa katika ajali hiyo ni pamoja na wanawake wanne na wanaume watano, na sasa majeruhi wamelazwa katika hospitali ya serikali ya Iringa wakipokea matibabu.