Maonesho ya chakula ya Afrika yafunguliwa Misri
2021-12-14 09:05:04| CRI

Maonesho ya sita ya kimataifa ya mazao ya chakula barani Afrika yalifunguliwa jumatatu mjini Cairo nchini Msiri, waonyeshaji zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali duniani wakihudhuria.

Maonesho hayo ya siku tatu yanayofanyika katika Kituo cha Maonesho cha Kimataifa, yanatarajiwa kuhudhuriwa na wataalam wapatao 21,000 wanaotafuta fursa za biashara.

Mahmoud Shabana, mkurugenzi wa mauzo nje wa kampuni moja ya chai ya Misri, amesema maonesho hayo ni jukwaa zuri kwa kampuni kukutana na wateja wapya kutoka nchi mbalimbali, na kuwasaidia kupata masoko mapya nje ya nchi.