Kenya yaanzisha kampeni ya chanjo ya siku mia moja dhidi ya surua na saratani ya shingo ya uzazi
2021-12-15 09:38:34| cri

Kenya imeanzisha kampeni ya siku mia moja ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua na saratani ya shingo ya uzazi kwa ajili ya watoto wenye umri wa miezi 18-59 na wasichana wa umri wa miaka 10-14.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa wizara ya afya ya Kenya Bw. Patrick Amoth alisema utoaji wa chanjo za kusaidia kinga ya mwili zimepunguza vifo na magonjwa kutokana na maradhi ya maambukizi ya utotoni kwa asilimia 70, lakini sasa chanjo dhidi ya surua na saratani ya shingo ya uzazi imewafikia asilimia 30-50 tu ya walengwa ambapo watoto wasiopungua laki 3 nchini humo wanakosa chanjo muhimu mbalimbali kila mwaka.

Bw. Amoth alishawishi wazazi wote kuhakikisha watoto kupewa chanjo hizo ambazo zimesambazwa katika vituo vya afya nchini kote.