Wataalamu wa Tehama wa Afrika watoa wito kuimarisha usalama wa watoto katika mtandao wa Internet
2021-12-15 09:27:41| CRI

Wataalamu wa teknolojia ya habari wa Afrika wametoa wito kuimarisha hatua, ili kuhakikisha watoto ni salama katika mtandao wa Internet wakati maambukizi ya COVID-19 yakiwahimiza watu zaidi kutumia mtandao huo.

Mkurugenzi mkuu wa idara ya mawasiliano ya Kenya Bw. Ezra Chiloba amesema, kutokana na kizuizi cha shughuli za kijamii na kufungwa kwa muda kwa shule, watoto wamegeukia njia za kidijitali kwa ajili ya michezo, mawasiliano na burudani na kusababisha ongezeko la hatari katika mtandao wa Internet.

Amesema hayo katika kongamano la mtandao wa Internet kuhusu ulinzi na usalama wa watoto, huku akiongeza kuwa hatua zinahitajika kuwalinda watoto kwenye mtandao wa Internet dhidi ya unyanyasaji na ukatili.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la kimataifa la polisi wa uhalifu wa jinai Interpol, mwaka jana kati ya asilimia 5 na 13 ya watoto wanaotumia mtandao wa Internet walikumbwa na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji mtandaoni.