Cameroon yapata dozi milioni 1 za chanjo ya COVID-19 kutoka China
2021-12-15 09:27:06| CRI

Shehena ya dozi milioni 1 za chanjo ya COVID-19 ya Sinopharm iliyotolewa na serikali ya China imewasili kwenye uwanja wa ndege wa Nsimalen huko Yaounde, mji mkuu wa Cameroon.

Konsela wa uchumi wa biashara wa ubalozi wa China nchini Cameroon Bw. Guo Jianjun na katibu mkuu wa mpango wa kupanua utoaji wa chanjo wa Cameroon Shalom Tchokfe Ndoula, walihudhuria hafla ya makabidhiano ya chanjo hizo.

Bw. Guo amesema kiwango cha utoaji wa chanjo barani Afrika ikiwemo Cameroon bado ni cha chini, na msaada huo kutoka China ni muhimu, wakati dunia ikiathiriwa vibaya na virusi vipya vya Corona ikiwemo Omicron. Katika mkutano wa 8 wa mawaziri wa FOCAC uliofungwa hivi karibuni, China iliahidi kutoa dozi bilioni 1 za chanjo kwa Afrika. Chini ya mfumo wa ushirikiano kati ya China na Afrika, ushirikiano wa afya na mapambano ya pamoja dhidi ya COVID-19 kati ya nchi hizo mbili hakika utapata mafanikio halisi.