Benki ya dunia yasema uchumi wa Kenya umeanza kufufuka kutokana na sekta ya huduma kufanya vizuri
2021-12-15 09:04:22| CRI

Ripoti iliyotolewa na benki kuu ya dunia inaonyesha kuwa uchumi wa Kenya umeonyesha nguvu ya uhai na kuongezeka zaidi ya viwango vilivyokuwepo kabla ya janga la COVID-19, ongezeko ambalo limechochewa na kurudi kwa nguvu kwenye sekta ya huduma.

Makadirio kuhusu uchumi wa Kenya (KEU) yanaonyesha kuongezeka kwa sekta ya huduma, kutokana na uungwaji mkono mkubwa wa sekta ya elimu. Sekta ndogo zenye mahitaji ya juu ya ujuzi pia yameshuhudia ongezeko kubwa la ajira, licha ya kuwa sekta zinazohitaji ujuzi mdogo bado zinatawala soko la ajira.

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Kenya Bw. Keith Hansen amesema licha ya ongezeko hilo, umaskini nchini Kenya umeongezeka, na njia za kukabiliana na hali ngumu kwenye kaya, makampuni na hata fedha za umma zimekwisha.