Msomi wa Mali: China na Afrika zapaswa kushirikiana kuongeza sauti na ushawishi ili kuelezekea hali halisi ya ushirikiano waokati yao
2021-12-16 14:08:04| CRI

Msomi wa Mali: China na Afrika zapaswa kushirikiana kuongeza sauti na ushawishi ili kuelezekea hali halisi ya ushirikiano waokati yao_fororder_Yoro

Msomi kutoka Mali Profesa Yoro Diallo  amesema, China na Afrika zinapaswa kushirikiana kwa karibu zaidi kuongeza sauti na ushawishi wao kwenye jukwaa la kimataifa, ili kuweza kuelezea sura halisi ya ushirikiano wao wa kunufaishana.

Profesa Yoro Diallo ambaye ni mtafiti mwandamizi wa Taassisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amesema, ni rahisi kwa watu na vyombo vya habari vya Afrika kuathiriwa na propaganda za nchi za magharibi, ambazo zinalenga kudhibiti mawazo ya watu wa Afrika, na hivyo kuleta mashaka na uelewa potofu kuhusu vitendo vya China barani Afrika. Amesema, China na Afrika zinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya watu wa kawaida na vyombo vya habari, kuongeza sauti na ushawishi wao kwenye jukwaa la kimataifa, ili kuweza kuelezea hali halisi ya ushirikiano mzuri kati ya pande hizo mbili.

Profesa Diallo anaona, Waraka Mweupe uitwao “Ushirikiano Kati ya China na Afrika Katika Zama Mpya” uliotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali ya China, umefafanua vizuri ushirikiano halisi wa pande hizo mbili katika zama mpya, na kuonesha kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika ni mfano wa kuigwa kwa ushirikiano wa Kusini-Kusini. Amesema, waraka huo umejibu kwa nguvu shutumua zisizo na msingi zilizotolewa na baadhi ya nchi za magharibi dhidi ya ushirikiano kati ya China na Afrika.

Profesa Diallo amesema, kwenye mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwezi Novemba nchini Senegal, China ilitoa mapendekezo manne kuhusu kujenga Jumuiya yenye Hatma ya Pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya, na kutangaza Miradi Tisa ya ushirikiano katika siku zijazo. Kuanzia afya ya umma hadi uhimizaji wa biashara, uvumbuzi wa kidijitali hadi amani na usalama, hatua hizo za China zimeitikia matarajio ya pamoja ya viongozi wa nchi za Afrika na wananchi wao. Profesa Diallo alimnukuu rais Macky Sall wa Senegal akisifu misaada ya dhati inayotolewa na China kwa Afrika, na kuona hii inaonesha mshikamano na undugu kati ya pande hizo mbili.