Jumuiya ya PACJA yazindua mradi wa kuhimiza upatikanaji wa nishati safi
2021-12-16 09:05:52| CRI

Jumuiya ya haki ya mabadiliko ya tabianchi ya Afrika (PACJA) yenye makao makuu yake mjini Nairobi, jana Jumatano ilizindua mradi wa kuhimiza upatikanaji wa vyanzo safi vya nishati barani humo ikiwa ni sehemu ya mpito wake wa kijani.

Mkurugenzi mtendaji wa PACJA Bw. Mithika Mwenda,, amesema mradi huo utakaotekelezwa kwa pamoja na jumuiya ya washauri bingwa wa sera za tabianchi ya Germanwatch, utatoa suluhu ya kudumu kwa umaskini wa nishati barani Afrika.

Bw. Mwenda amesema upatikanaji wa nishati safi ni muhimu katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu yanayohusiana na usalama wa chakula, umaskini, afya, usawa wa kijinsia, elimu na mazingira.