China yatoa tani zaidi 400 za mchele kwa Sudan Kusini
2021-12-16 09:35:17| CRI

Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umetoa msaada wa dharura wa tani 416 za mchele kwa majimbo yaliyoathiriwa na mafuriko nchini humo.

Mwenyekiti wa tume ya utoaji wa misaada ya Sudan Kusini Bw. Manase Lomole alisema msaada huo unaonyesha kuwa China inaendelea kuwaunga mkono watu wa Sudan Kusini. Amesema kuanzia mwaka jana Sudan Kusini imesumbuliwa na mafuriko makubwa kabisa katika miaka 60 iliyopita, na watu zaidi 800,000 wameathiriwa na mafuriko katika majimbo manane, huku wengine milioni 11 bado wakikabiliwa na uhaba wa chakula.

Bw. Lomole ameishukuru China kwa mchango na msaada wake katika sekta ya afya na huduma za kibinadamu kwa nchi hiyo.