Soko la China laleta matumaini mauzo ya nje ya kakao ya Ghana
2021-12-16 09:33:18| cri

China imeleta matumaini kwa mazao ya kakao kutoka Ghana kuingia kwenye soko lake, wakati uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukizidi kuimarika.

Mtendaji mkuu wa kampuni Niche Cocoa moja ya kampuni zinazochakata kakao nchini Ghana Bw. Nathaniel Durant, amesema soko la China linaweza kuwa soko muhimu kwa mauzo nje ya maharagwe ya kakao na bidhaa mbalimbali za kakao na kuileta faida kubwa Ghana na wakulima wake.

Pia ameongeza kuwa mbinu ya kuingia katika soko la China si lazima kutumia njia ya zamani ya kuangalia matumizi ya kila mtu au idadi ya watu kubainisha uwezo wa soko. Ameshauri wafanyabiashara kuelewa kwanza upendeleo wa watumiaji wa China kuhusu ladha ya kakao na mzunguko wa matumizi, na hata mwonekano wa bidhaa ya kakao.