Kampuni ya China yaanza maandalizi ya kujenga bwawa jipya ili kutoa maji mjini Harare
2021-12-17 08:58:49| CRI

Kampuni ya uhandisi ya Nanchang kutoka China inajiandaa kujenga mradi wa bwawa la Kunzvi wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 109 kwenye eneo la Goromonzi mkoani Mashonaland Mashariki, ambao utakuwa chanzo kipya cha maji kwa mji mkuu wa Zimbabwe Harare.

Bwawa hilo litakalojengwa kaskazini mashariki mwa mji huo, litauondolea mji wa Harare tatizo la kukosa vyanzo vya maji safi, ambavyo viwili kati ya vyanzo vinne vilivyopo vimechafuliwa vibaya.

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald, wakazi wa huko na viongozi wa jadi wamekaribisha maendeleo mapya ya mradi huo, ambao utaboresha maisha yao wakati miradi mingine kama vile ya umwagiliaji inapangwa.