Tanzania kuweka maabara za kompyuta shuleni ili kuimarisha sekta ya tehama
2021-12-17 09:27:54| CRI

Waziri wa nchi ofisi ya rais wa Tanzania anayeshughulikia tawala za mikoa na serikali za mitaa Bibi Ummy Mwalimu, ametangaza kuwa shule zote mpya za sekondari za umma zitawekwa maabara za kompyuta ili kuwawezesha walimu kufundisha teknolojia ya habari na mawasiliano na kuimarisha elimu hiyo.

Bibi Mwalimu amesema serikali ya Tanzania inalenga kuweka maabara za kompyuta na vifaa vya tehama katika shule mpya 1,500 za sekondari ndani ya miaka mitatu kuanzia mwaka 2022.