Tanzania yataka ushirikiano katika utunzaji wa Ziwa Tanganyika
2021-12-17 09:32:11| cri

Makamu wa Rais wa Tanzania Philip Mpango ametoa wito kwa nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika kuchukua hatua za kupunguza uharibifu wa mazingira katika ziwa hilo, ambalo ni ziwa la pili la maji baridi lenye historia ndefu zaidi duniani.

Amesema nchi husika zikiwemo Burundi, Congo DRC na Tanzania zinatakiwa kushirikiana kutunza anuwai ya viumbe hai wa ziwa hilo iliyoharibiwa kutokana na shughuli za uvuvi na kilimo cha kupita kiasi, uchafuzi wa maji na ukataji miti.

Bw. Mpango aliongeza kuwa ziwa hilo linatakiwa kuwa na uwezo wa kutoa samaki tani milioni 1.5 za ujazo kila mwaka, lakini sasa ni laki 5.8 zimepatikana tu kutokana na uharibifu wa mazingira.