Watu 12 wauawa na marahamia kaskazini mwa Kenya
2021-12-20 09:02:19| CRI

 

 

Watu 12 wameuawa baada ya maharamia kushambulia vijiji vilivyoko kwenye Kaunti ya Marsabit, kaskazini mwa Kenya Jumamosi iliyopita.

Kamanda wa polisi katika kaunti hiyo Robinson Mboloi amesema, maharamia hao waliokuwa na silaha pia walitoroka na idadi kubwa ya mifugo. Amesema timu ya pamoja kutoka taasisi za usalama inaendelea na msako dhidi ya wanyang’anyi hao, na kuongeza kuwa ushirikiano kutoka kwa umma ni muhimu katika kumaliza wizi wa mifugo kaskazini mwa Kenya.

Hivi karibuni, Kaunti ya Marsabit imeshuhudia vitendo vya unyang’anyi na mapigano ya kikabila yanayohusishwa na kugombania rasilimali ya maji na maeneo ya malisho.