Naibu mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Umoja wa Afrika, Erastus Mwencha amesema, pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja linaendana na ajenda ya maendeleo ya mwaka 2063 ya Umoja huo, na linaharakisha uboreshaji wa miundombinu na muungano wa soko barani Afrika.
Mwencha amesema, pendekezo hilo linafuata maslahi ya maendeleo ya Afrika, na litaleta teknolojia na mitaji kwa Afrika katika kuendeleza uchumi wa kidijitali, kuongeza uwezo wa uzalishaji bidhaa, kuhimiza uhamishaji wa teknolojia, kuhamasisha uwekezaji kwa sekta zisizosababisha uchafuzi, na kukuza mawasiliano ya watu na utamaduni.
Amesema, utekelezaji wa mfululizo wa miradi ya Ukanda Mmoja, Njia Moja, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli, bandari, na miundombinu ya kidijitali, umebadilisha sura ya Afrika kuboresha maisha ya watu barani humo.