Walimu na wanafunzi 123 wa Tanzania watunukiwa "Tuzo ya Balozi wa China"
2021-12-20 08:27:25| cri

Ubalozi wa China nchini Tanzania hivi karibuni ulifanya hafla ya 4 ya "Tuzo ya Balozi wa China", ambapo jumla ya walimu na wanafunzi 123 wa Tanzania walipewa tuzo hiyo mwaka huu.

Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Chen Mingjian amewapongeza walimu na wanafunzi hao na kusema, mwaka huu serikali ya Tanzania imefanya mageuzi ya mfumo wa shule za sekondari na kuorodhesha lugha ya Kichina katika mfumo wa elimu wa taifa. Hatua hiyo muhimu imeendana na matarajio ya watu na mahitaji ya maendeleo ya jamii, na ni matokeo mengine muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia nchini Tanzania Profesa Joyce Ndalichako ameishukuru China kwa juhudi zake katika kuendeleza ushirikiano wa elimu kati ya nchi hizo mbili na kuwapongeza washindi wote wa tuzo hiyo.