Gazeti la New York Times ladokeza kwamba idadi ya raia waliouawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani ni kubwa zaidi kuliko makadirio
2021-12-20 14:12:02| cri

Gazeti la New York Times la Marekani tarehe 18 lilichapisha makala ikifichua nyaraka zaidi ya 1,300 za siri za Wizara ya Ulinzi ya Marekani kuhusu vifo vya raia waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Marekani. Nyaraka hizi zinabainisha kuwa mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Marekani katika Mashariki ya Kati tangu mwaka 2014 yana makosa mengi, yamefanywa kwa pupa na mara nyingi kufanywa katika sehemu zisizo sahihi, hivyo yalisababisha vifo vya maelfu ya raia wasiokuwa na hatia, wengi wao ni watoto. Hili ni jambo linalokwenda kinyume kabisa kwa serikali ya Marekani kujiita wafanya"mashambulizi ya usahihi".

Ingawa hata jeshi la Marekani linakubali kusababisha vifo vya raia, lakini idadi ya vifo vya raia mara nyingi inakuwa ni kubwa zaidi kuliko makadirio. Watu wengi walionusurika walipata ulemavu na walihitaji matibabu ya gharama kubwa, lakini Marekani ililipa chini ya mara 12 tu.