Watu 40 wauawa katika mashamblizi kaskazini mwa Nigeria
2021-12-21 08:45:47| cri

 

 

Kamishna wa mambo ya usalama wa ndani katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria Bw. Samuel Aruwan jana amesema, idadi ya vifo kutokana na mashambulizi yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika vijiji vya jimbo hilo imeongezeka na kufikia 40 baada ya miili miwili zaidi kupatikana.

Bw. Aruwan amesema, vijiji vya Kauran Fawa, Marke na Riheya katika eneo la Giwa vilishambuliwa na watu wenye silaha kati ya Jumamosi usiku na Jumapili asubuhi.

Mashambulizi ya silaha yamekuwa tishio kubwa la usalama katika mikoa ya kaskazini na katikati mwa Nigeria, na kusababisha vifo na utekaji nyara.