Watu zaidi ya 17 wafariki katika ajali ya meli nchini Madagaska
2021-12-21 08:43:47| cri

Watu zaidi ya 17 wamefariki na wengine 60 hawajulikani walipo baada ya meli iliyokuwa ikitokea kaskazini mashariki mwa Madagaska kupinduka na kuzama.

Meli hiyo iliyokuwa imebeba abiria 130, iliondoka Antanambe jana, maji yaliingia kwenye chumba cha injini wakati meli ikiwa njiani kuelekea Suanierana-Iungu na kusababisha meli hiyo kuzama.

Habari zinasema, meli hiyo ilikuwa ni meli ya mizigo na haikuwa na leseni ya kubeba abiria, na pia ilianza safari yake kutoka bandari isiyotambulika ya serikali.