Watu wanne wauawa katika mapigano kaskazini mashariki mwa DRC
2021-12-21 08:53:28| CRI

Askari polisi watatu na raia mmoja wameuawa katika mapigano kati ya waandamanaji na polisi yaliyotokea kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana asubuhi.

Kituo cha Radio Okapi kinachoungwa mkono na Kikosi cha kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) kimesema, mvutano umekuwa ukiongezeka kufuatia shambulizi lililotokea Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini tangu jumatatu, kutokana na kuongezeka kwa uhalifu kwenye kanda hiyo na tishio la uwepo wa polisi wa Rwanda nchini DRC.

Polisi wa huko wamethibitisha vifo hivyo, na kuongeza kuwa askari polisi wamepelekwa kwenye eneo hilo kusaidia kudhibiti hali ya usalama.