Waziri Mkuu wa Somalia atoa wito wa mazungumzo ya kiujenzi kuongeza kasi ya mchakato wa uchaguzi nchini humo
2021-12-22 08:14:13| CRI

Waziri Mkuu wa Somalia atoa wito wa mazungumzo ya kiujenzi kuongeza kasi ya mchakato wa uchaguzi nchini humo_fororder_索马里总理Robel

Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Roble ametoa wito wa mazungumzo ya kiujenzi ya kitaifa yanayolenga kuongeza kasi ya mchakato wa uchaguzi.

Roble, ambaye amepewa jukumu la kusimamia uchaguzi huo, amesema mkutano utakaokutanisha serikali na wawakilishi wa mikoa mitano ya nchi hiyo utafanyika mjini Mogadishu Desemba 27.

Katika taarifa yake, Roble amesema mkutano huo utajikita katika kuongeza kasi ya mchakato wa uchaguzi, na kurekebisha na kukamilisha mchakato huo.

Taarifa hiyo imekuja wakati uchaguzi wa wabunge ulioanza mwezi Novemba ukiendelea vizuri ingawa kwa taratibu, katika mikoa yote ya kiutawala nchini humo.