Rais wa Kenya aahidi kuendeleza maingiliano ya kikanda
2021-12-23 08:55:42| CRI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameahidi kuendeleza mchakato wa maingiliano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akisema Jumuiya hiyo ni jukwaa la msingi kwa mageuzi ya kiuchumi na kijamii katika kanda hiyo.

Rais Kenyatta amesema hayo alipoendesha mkutano maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao, akieleza kuridhishwa na maendeleo yaliyopatikana kuelekea mshikamano zaidi na ustawi wa pamoja wa kikanda.

Mkutano huo pia ulijadili ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) la kujiunga na Jumuiya hiyo. Rais Kenyatta amelitaka Baraza la Mawaziri wa EAC kuharakisha mchakato wa kuikubalia DRC kuwa nchi mwanachama wa Jumuiya hiyo.