Zaidi ya watu milioni 3.2 nchini Somalia waathiriwa na ukame
2021-12-23 09:00:01| CRI

Zaidi ya watu milioni 3.2 nchini Somalia waathiriwa na ukame_fororder_VCG31502436557

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uratibu wa masuala ya kibinadamu (UNOCHA) imesema, zaidi ya watu milioni 3.2 katika wilaya 66 nchini Somalia wameathiriwa na ukame wa kihistoria ulioendelea kwa misimu mingi.

Ripoti iliyotolewa na UNOCHA pia imesema, takriban watu 169,000 wamekimbia makazi yao ili kutafuta chakula, maji na malisho ya mifugo.

Ofisi hiyo imesema, washirika wa kibinadamu wameandaa mpango wa miezi sita wa kukabiliana na ukame nchini Somalia ili kupunguza athari zinazozidi kuwa mbaya na kuongeza juhudi za kukusanya rasilimali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Umoja wa Mataifa na washirika wengine wa masuala ya kibinadamu kuzindua Mpango wa Kibinadamu kwa mwaka 2022, ambao unalenga kukusanya takriban dola bilioni 1.5 za kimarekani ili kuwasaidia watu milioni 5.5 walio hatarini zaidi nchini Somalia.