Watu zaidi ya 83 wafariki katika ajali ya meli nchini Madagascar
2021-12-23 08:58:37| cri

Watu zaidi ya 83 wamefariki, 50 waokolewa na wengine watano hawajulikani walipo baada ya meli iliyokuwa ikitokea kaskazini mashariki mwa Madagascar kupinduka na kuzama.

Habari zinasema, shughuli za uokoaji na uchunguzi wa ajali hiyo zilisitishwa jana mchana kutokana na hali mbaya ya hewa na zinatarajiwa kuendelea leo asubuhi.