Jeshi la Ethiopia latakiwa kuthibiti maeneo linaloshikilia bila kusonga mbele
2021-12-24 08:46:24| CRI

Serikali ya Ethiopia jana imetangaza mafanikio makubwa ya operesheni ya jeshi lake dhidi ya waasi katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Shirika la Utangazaji la Fana (FBC) nchini Ethiopia limemnukuu Waziri wa Huduma za Mawasiliano ya Serikali nchini humo Legesse Tulu akisema, vikosi vya jeshi la serikali vimeondoa makundi ya magaidi katika mikoa ya Afar na Amhara, na kuzuia kundi la waasi kuchukua silaha zilizoletwa na magaidi hao.

Ameongeza kuwa, serikali imetoa amri kwa jeshi lake kushikilia maeneo waliyokomboa bila ya kusonga mbele kutokana na sababu mbalimbali.