Sudan yawakamata waandamanaji 114 kwa kukiuka sheria kwenye maandamano
2021-12-27 10:10:20| CRI

Sudan yawakamata waandamanaji 114 kwa kukiuka sheria kwenye maandamano_fororder_3

Mamlaka za usalama nchini Sudan zimewakamata waandamanaji 114 kwa kukiuka sheria wakati wa maandamano yaliyofanyika Jumamosi katika mji mkuu Khartoum.

Kamati ya Uratibu wa Mambo ya Usalama wa Taifa imesema kwenye taarifa yake kwamba watuhumiwa wote watachukuliwa hatua za kisheria. Sheria walizokiuka ni pamoja na kushambulia jengo la ukaguzi la Nile mashariki, jaribio la shambulizi kwenye kituo cha polisi cha mji wa Bahri, kuvunja madirisha ya magari manne ya polisi, na kuharibu sakafu, mabango na alama za barabarani.

Kamati imesisitiza kuwa polisi wanaoshughulikia vurugu watumie nguvu za wastani pamoja na gesi za kutoa machozi.