Mkuu wa UM aomboleza kifo cha askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu
2021-12-27 10:09:14| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jana aliomboleza kifo cha askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu, akimwita mnara wa amani duniani, sauti isiyoyumba ya watu na msukumo kwa vizazi vyote duniani.

Kwenye taarifa yake Bw. Guterres alisema wakati wa ubaguzi wa rangi alikuwa taa inayong’aa kwa haki ya kijamii, uhuru na kufanya upinzani usio na vurugu. Aidha azma ya askofu Tutu ya kujenga mshikamano duniani bila kuchoka kwa ajili ya uhuru na demokrasia ya Afrika Kusini ilifaa kabisa kutambuliwa na kamati ya Nobel wakati ilipoamua kumtunuku Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1984. Akiwa kama mwenyekiti wa Tume ya Ukweli na Mapatano alitoa mchango mkubwa kuhakikisha amani nchini Afrika Kusini ambayo ilikuwa ndio kwanza kwenye kipindi cha mpito cha demokrasia.