Polisi ya Uganda yapiga marufuku kupiga fataki wakati wa sikukuu ya mwaka mpya
2021-12-28 09:42:27| CRI

Polisi nchini Uganda jana ilitangaza kuwa ni marufuku kupiga fataki wakati wa sikukuu ya mwaka mpya itakayokuwa wikiendi hii.

Msemaji wa polisi ya Uganda Fred Enanga amesema kwa mwaka wa pili sasa fataki zimepigwa marufuku kutokana na hali ya kutokuwa na uhakika inayosababishwa na janga la Corona. Enanga amesema wananchi wanaweza kusherehekea mwaka mpya kwa makundi madogo badala ya mikusanyiko mikubwa ambayo inaweza kusababisha kuenea kwa virusi vya Corona.

Ameongeza kuwa sala za usiku za kukaribisha mwaka mpya makanisani pia zimepigwa marufuku ili kuzuia mkusanyiko wa watu. Kwa kuwa mwaka mpya utaingia wakati wa kipindi cha marufuku ya kutoka nje usiku, hivyo polisi itachukua hatua kali zaidi kwenye muda huo.