DRC yazindua kampeni ya chanjo ya kipindupindu ikilenga watu milioni 2
2021-12-28 09:43:23| CRI

DRC yazindua kampeni ya chanjo ya kipindupindu ikilenga watu milioni 2_fororder_霍乱

Maafisa wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamesema nchi hiyo imezindua kampeni ya chanjo ya kipindupindu Jumatatu, ikilenga watu wengi zaidi wapatao milioni 2 wenye umri wa mwaka mmoja na kuendelea katika majimbo matatu ya mashariki ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Kampeni hiyo itakayoendelea kwa siku sita inaendeshwa kwenye majimbo ya Haut-Lomami, Kivu Kusini na Tanganyika, ambayo yameathirika zaidi na kipindupindu tangu mwezi Agosti, na itafanyika kwenye maeneo 13 ya afya huku zikitolewa dozi milioni 4 na Global Task Force inayodhibiti kipindupindu. Watumishi wa afya 3,600 wakiwemo watoa chanjo na wahamasishaji wa kijamii wamesambazwa ili kuendeleza kampeni hiyo.

Tangu kuanza kwa kipindupindu, DRC imeripoti jumla ya watu wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huo wapatao 8,279 na vifo 153 kwenye majimbo 16 kati ya 26 ya nchi hiyo.