Nchi za Magharibi zinatakiwa kuacha utaifa wa chanjo
2021-12-29 09:54:36| CRI

Hivi karibuni, Nigeria iliteketeza dozi milioni 1.06 za chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca iliyokwisha muda wake. Wakati virusi vipya vya Corona Omicron vinaenea haraka duniani kote, jambo hilo lililotokea katika nchi ya Afrika, ambako kuna uhaba mkubwa wa chanjo na idadi ndogo ya watu waliopata cjanjo hiyo, linashangaza sana watu.

Habari zinasema shehena hiyo ya chanjo iliingia barani Afrika kutoka nchi moja ya Ulaya kupitia Mpango wa Utekelezaji wa Chanjo (COVAX). Wakati ilipofika nchini Nigeria, muda wa chanjo hiyo ulikuwa umebaki wiki 4 hadi 6 tu, na kuifanya nchi hiyo ishindwe kuitoa kwa raia wake kwa wakati. Mkuu wa Kamati Kuu ya utoaji wa chanjo nchini Nigeria, Dkt. Faisal Shuaib amelalamika kuwa, “nchi zilizoendelea zilitengeneza chanjo hizo, halafu zilizilimbikiza, na kuzitoa wakati muda wake ulipokaribia kumalizika.”

Tukio hilo si kipekee barani Afrika. Habari zinasema kabla ya hapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imerejesha dozi milioni 1.3 za chanjo kwa nchi za Magharibi kwa sababu muda wa chanjo hizo unakaribia kwisha, na Senegal imetangaza kuteketeza dozi laki nne za chanjo zilizoisha muda wake kabla ya mwishoni mwa mwaka huu. Zaidi ya hayo, nchi nyingine za Afrika zikiwemo Malawi, Sudan Kusini, Liberia, Mauritania, Gambia, Sierra Leone, Guinea, Comoro na Jamhuri ya Kongo pia zimeteketeza chanjo zilizokwisha muda wake zilizotoka nchi za Magharibi. Hii ni hasara kubwa kwa Afrika, ambapo kiwango cha watu waliopewa chanjo ya COVID-19 hadi sasa kimekuwa asilimia 5 tu. Ili kubadilisha hali hiyo, tawi la COVAX barani Afrika hivi karibuni limetoa wito wa kutoa chanjo yenye ubora kwa Afrika.

Ufujaji wa chanjo barani Afrika unatokana na “utaifa wa chanjo” wa nchi za Magharibi. Wakati chanjo dhidi ya COVID-19 ilikuwa bado katika hatua ya ubunifu mwaka jana, nchi hizo haswa Marekani zilianza kuiagiza kwa wingi. Baada ya chanjo hizo kuwa tayari, licha ya kukidhi mahitaji ya ndani, badala ya kuigawa kwa nchi nyingine zenye mahitaji ya haraka, nchi hizo zimeilimbikiza kwa wingi kupita kiasi, mpaka chanjo hiyo inakaribia kuisha kwa muda. Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa nchini Marekani na katika nchi nyingine za Magharibi kuna takriban dozi milioni 240 za chanjo ambayo muda wake unakaribia kuisha. Hivyo zinafikiria kuchangia au hata kuuza chanjo hizo kwa nchi nyingine, haswa nchi za Afrika, ili “kutimiza” ahadi yao ya kuchangia nchi zinazoendelea chanjo dhidi ya COVID-19.

Maofisa wa COVAX wamesema, misaada mingi ya chanjo kutoka nchi za Magharibi kwa Afrika ni ya haraka, na bila ya kupangwa vizuri, na muda wa chanjo hizo nyingi unakabiria kuisha.

Kwa upande mwingine, hadi sasa China imetoa zaidi ya dozi milioni 180 za chanjo ya COVID-19 kwa nchi 53 za Afrika na Umoja wa Afrika. Ni tofauti na nchi za Magharibi, chanjo hizo zimetolewa kwa Afrika wakati zinatumiwa nchini China. Katika mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hivi karibuni nchini Senegal, Rais Xi Jinping wa China aliahidi kutoa dozi nyingine milioni 100 za chanjo kwa Afrika, na kati yao dozi milioni 600 ni msaada, na nyingine milioni 400 zitatolewa kwa njia ya ushirikiano wa uzalishaji kati ya kampuni za China na nchi za Afrika.

Virusi havijali mipaka. Maambukizi ya virusi vya Corona yaliyokabili dunia kwa miaka miwili yameonesha umuhimu wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Nchi za Magharibi zinatakiwa kuacha “utaifa wa chanjo”, na kuanza kujitahidi kujenga kinga ya chanjo dhidi ya virusi vya Corona duniani kote, ili kumaliza kabisa janga la COVID-19.