Ethiopia yasajili wagonjwa 4,998 wapya wa COVID-19
2021-12-31 20:09:21| CRI

Wizara ya afya ya Ethiopia imesema nchi hiyo imesajili wagonjwa 4,998 wapya wa COVID-19 katika saa 24 zilizopita, ikiongeza idadi ya jumla ya wagonjwa kote nchini kufikia 415,433 hadi kufikia jioni ya Alhamisi.

Wizara hiyo imeripoti vifo 10 vipya vinavyohusiana na COVID-19 na wagonjwa 321 waliopona, na kufanya idadi ya jumla ya vifo na watu waliopona kufikia 6,926 na 354,495 mtawalia.

Ethiopia ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, ambayo pia ni nchi inayoripoti wagonjwa wengi zaidi wa COVID-19 huko Afrika Mashariki. Wizara hiyo imesema katika mchakato wa kuhimiza utoaji wa chanjo nchini humo, Ethiopia imetoa dozi 10,914,333 za chanjo ya COVID-19.