Waziri wa mambo ya nje wa China kuizuru Afrika kwanza mwanzoni mwa mwaka mpya wa 2022
2021-12-31 10:13:01| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China kuizuru Afrika kwanza mwanzoni mwa mwaka mpya wa 2022_fororder_访非头图

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi atatembelea nchi za Eritrea, Kenya na visiwa vya Comoro kutokana na mialiko kuanzia Januri 4 hadi 7 mwaka 2022.

Bw. Zhao ameeleza kuwa, ziara hiyo katika nchi tatu barani Afrika inadumisha desturi ya waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara ya kwanza ya kila mwaka barani Afrika katika miaka 32 iliyopita, pia imeonesha utiliaji maanani mkubwa wa China juu ya urafiki wa jadi kati ya China na Afrika pamoja na maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbili. Amesema katika miaka ya hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China alipohutubia Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika nchini Senegal, ametoa wito wa kuenzi moyo wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika na kukaribishwa na upande wa Afrika.

Pia amesema Bw. Wang Yi atafanya tena ziara Afrika baada ya mwezi mmoja, ikiwa na lengo la kutekeleza matokeo yaliyopatikana katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kujadiliana kwa kina utekelezaji wa hatua mpya za ushirikiano, na kuziunga mkono nchi za Afrika kushinda mapema katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19 na kutimiza ufufukaji wa uchumi, hatua ambayo imeonesha tabia ya China ya kutekeleza ahadi kwa vitendo halisi.

Bw. Zhao Lijian pia amesisitiza kuwa, mabadliko ya hali ya kimataifa na hali ya maambukizi ya COVID-19, hayatazuia China na Afrika kudumisha mawasiliano ya kirafiki, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na imani ya kusaidiana, pamoja na uungaji mkono wa China kwa nchi za Afrika. Hii vilevile ni nia inayostahiki katika kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika enzi mpya.