Mwenyekiti wa AU atoa wito wa kujizuia nchini Somalia
2021-12-31 10:10:51| CRI

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ameeleza wasiwasi wake juu ya mvutano unaonedelea nchini Somalia.

Bw. Mahamat ametoa wito wa kujizuia kabisa na kuwasisitiza rais wa nchi hiyo na waziri mkuu wake kuendelea kushiriki kwenye mazungumzo ili kupata ufumbuzi wa kisiasa wa mvutano uliopo sasa. Kufuatia mvutano wa kisiasa unaoendelea kukua nchini humo, rais wa Somalia Muhamed Farmajo alimsimamisha kazi waziri wake mkuu Mohamed Roble kutokana na madai ya ufisadi.

Kwenye taarifa yake aliyoitoa siku moja baada ya kumshutumu Roble kwa kushindwa kuongoza mchakato wa uchaguzi na kupata mafanikio, Farmajo pia anamshutumu Roble kwa kujihusisha na ufisadi na matumizi mabaya ya ardhi ya umma.