Wanamichezo wa Afrika wapinga kufanya michezo kuwa jambo la kisiasa
2021-12-31 18:53:09| CRI

Mwenyekiti wa Shirikisho la wanamichezo wa Afrika Hamad Kalkaba Malboum ametoa mwito wa kufanya juhudi kuzuia siasa kuingilia mambo ya michezo.

Bw. Malboum ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya taifa ya olimpiki na michezo ya Cameroon, amesema michezo haina siasa, na ni njia inayovuka ubinafsi ili kuwafanya vijana duniani wakusanyike mahali pamoja bila kujali tofauti za lugha, rangi na utamaduni. Amesema kwa sasa wanataka kutoa ujumbe wa amani, wa dunia inayokalika, kwa hiyo mambo ya siasa yanatakiwa kuwekwa pembeni.

Bw. Malboum ameipongeza China kwa juhudi ilizofanya kuandaa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, na kusema michezo hiyo itakuwa mkusanyiko muhimu wa kuonyesha mshikamano wa dunia dhidi ya janga la COVID-19, na kutoa ujumbe chanya kuwa binadamu watashinda janga la COVID-19 kupitia juhudi za pamoja.