Watu wanne wauawa kwenye maandamano mjini Omdurman, Sudan
2021-12-31 10:07:02| CRI

Wizara ya afya iliyovunjwa jimboni Khartoum, Sudan imesema watu wanne waliuawa jana kwenye maandamano mjini Omdurman, baada ya jeshi kutumia silaha kali kwenye maandamano hayo.

Hapo awali, shirika lisilo la kiserikali Kamati kuu ya madaktari wa Sudan (CCSD) lilisema kwenye maandamano yaliyotokea mjini Omdurman watu watatu waliuawa kwa risasi zilizotumiwa na jeshi la mapinduzi na wanamgambo ambao ni washirika wao. Shirika hilo pia limesema mamlaka ya sasa inafanya mashambulizi mabaya dhidi ya wananchi, na shughuli za msako zinaendelea kufanyika kwenye jamii.

Hadi sasa, serikali ya Sudan bado haijatoa taarifa yoyote juu ya maandamano ya Alhamisi.